Diamond ampotezea Zuchu Instagram

Diamond ampotezea Zuchu Instagram

Mwanamuziki #DiamondPlatnumz amemu-Unfollow mpenzi wake Zuchu kwenye account yake ya Instagram baada ya hivi karibuni mrembo huyo kutoa kauli akidai kuwa amechoshwa kuvunjiwa heshima na Diamond.

Wawili hao wamekuwa katika ugomvi ambao unahusishwa na wivu wa mapenzi ambapo Zuchu amefikia hatua kukusanya virago vyake na kuondoka katika nyumba ambayo alikuwa anaishi pika pakua na Diamond akidai kuchoshwa na mahusiano hayo.

Licha ya msanii huyo kumu-Unfollow lakini Zuchu ameendelea kum-follow Diamond, hivyo kulingana na mambo yanavyoendelea baina yao huenda mahusiano hayo yakawa yamevunjika rasmi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags