Diamond ageukia kwenye fashion

Diamond ageukia kwenye fashion

Wakati Diamond Platnumz akiendelea kusherehekea mafanikio ya ngoma yake ya ‘Komasava’ Duniani, msanii huyo kuna namna kama amegeukia kwenye ulimwengu wa fashion hivi, hii ni baada ya ku-share mitindo mbalimbali ya mavazi.

Toka mwanamuziki huyo kuonekana katika maonesho ya mitindo ya ‘Paris Fashion Week’ yaliyofanyika nchini Ufaransa siku chache zilizopita, Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram amekuwa aki-share picha akiwa amevalia mavazi tofauti tofauti ya kimitindo.

Vazi la kwanza la msanii huyo ambalo lilipewa umakini ni la Pweza ambalo alilivaa katika maonesho hayo, vazi pili likiwa ni suti nyeusi aliyoivaa na miwani ambayo ilitrend sana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni tofauti na miwani nyingine.

La tatu likiwa ni koti kubwa lenye rangi ya silva lililokaa kama puto ambalo alivalishwa na Kyojino, mwanamitindo kutoka nchini Paris ambae mitindo yake imekuwa ikitumiwa na wasanii wengi kama vile Davido, Tyla, na wasanii wengine wengi. Huku vazi la mwisho alilolivaa leo ambalo ameliposti masaa machache yaliyopita.

Kama ni mfuatiliaji zaidi wa msanii huyo huwa sio mpenzi sana wa kutupia picha za kimitindo mbalimbali mitandaoni, haya tuambie ni mwonekano upi uliukubali zaidi kutoka kwa msanii huyo?.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags