Diamond aashinda tuzo ya Msanii Bora Afrika

Diamond aashinda tuzo ya Msanii Bora Afrika

Msanii wa muziki wa bongofleva na bosi wa lebal ya WCB, Nassibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo ya msanii bora wa Afrika mwaka 2021 katika tuzo za Ghana Music Awards Uk.

Katika kipengele hicho, Diamond alikuwa akishindana na wasanii wengine akiwemo Burna Boy, Davido, Wizkid, Master KG, Fireboy, Mercy Chinwo, Judikaya, Teni, Sinach na Patoranking.

Hafla za utoaji wa tuzo hizo zimefanyika usiku wa kuamkia leo huko jijini London Uingereza katika ukumbi wa Royal Regency.

Diamond pia yupo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za AFRIMA na AFRIMMA.

Kwa sasa Diamond yupo kwenye ziara yake nchini Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags