
Diamiond ajibu kiutu uzima ishi yake ya kufuturisha
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz amejibu lawama alizopewa na baadhi ya watu zikihusisha tukio la kufuturisha watu maarufu alilolifanya Machi 20, 2025.
Katika tukio hilo la kufuturisha lilipelekea baadhi ya watu kulitafsiri tofauti huku wengi wakionesha kutamani kuona msanii huyo akifuturisha watu wenye uhitaji tofauti na alivyofanya yeye.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 30,2025 Diamond amesema anafanya mema kadri Mungu anavyomjalia.
"Unajua inabidi ufanye kadri mwenyezi Mungu alivyokujaalia, alafu anayehukumu ni mwenyezi Mungu ukisikiliza maneno ya watu utashindwa kufanya mambo mazuri. Kwa kufikiria utaonekanaje, mimi namuomba Mungu nifanye mambo mazuri, na sishtuki sijali wala siogopi maoni ya mtu. Mimi jukumu langu ni kuona nimepata nafasi na nafasi hii inawafaidisha watu.
"Maoni ya watu hauwezi kuyaepuka, mimi sifanyi kwa sababu ya watu nafanya kwa sababu ya Allah, na uzuri hata sheikh wa Mkoa alilielezea vizuri kwa hiyo ni vitu vya kawaida na hata kwa watu wengine wanaofanya mambo msikatishwe tamaa,"amesema.
Diamond ameongezea kuwa licha ya yeye kuwa msanii lakini bado anafanya ibada swala tano mfululizo kwa mwaka wa tatu sasa.
"Hata kwa watu wengine wanaofanya mambo msikatishwe tamaa. Mwenyezi Mungu anasema msikate tamaa na neema zangu kwa hiyo asitokee kiumbe kukukatisha tamaa, haijalishi unafanya kazi gani. Hakikisha unaswali mimi naswali swala tano maisha yangu sasa hivi mwaka wa tatu kama utaniona mnafiki sawa," amesema.
Utakumbuka tukio hilo la kufuturisha lilihudhuriwa na wachekeshaji, waigizaji na wanamuziki.
Leave a Reply