Dereva achoma School Bus ikiwa na watoto 66

Dereva achoma School Bus ikiwa na watoto 66

Dereva wa bus la shule ya Utah kutoka nchini Marekani anayefahamika kwa jina la Michael Austin Ford mwenye umri wa miaka 58 amekamatwa na polisi kwa tuhumima za kuchoma bus la shule (school bus) lililokuwa na watoto 66.

Polisi walimkamata mwanaume huyo aliyekuwa akiendesha gari la Granite School siku ya jana Jumatatu ambapo anatuhumiwa kuchoma ma-bus mengi kwa miaka michache iliyopita, unyanyasaji wa watoto na uhalibifu wa mali.

Kutokana na tukio hilo uongozi wa shule hiyo umeeleza kuwa hakuna athari ya moto iliyompata mtoto kwani hakuna aliyejeruhiwa, wanafunzi walitumia milango ya dharura kunusuru maisha yao.

 Hata hivyo kwa mujibu wa vyombo vya habari vinaeleza kuwa Ford alifanya tukio hilo makusudi kwa kupuuzia usalama wake, wa watoto na umma baada ya camera kuonesha akiendesha gari huku likiwa linawaka moto.

Kufuatia file la kutunza matukio ya uhalifu polisi walieleza kuwa mwanaume huyo alihusishwa kwenye matukio ya moto nane katika miaka ya hivi karibuni moja wapo likiwa la Februari 24, 2022, huku jingine likiwa ni kuunguza nyumba na gari yake wiki iliyopita ambapo sababu ya kufanya matukio hayo bado haijajulikana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags