De Bruyne ashika rekodi ya mabao Man City

De Bruyne ashika rekodi ya mabao Man City

Kiungo mshambuliaji wa ‘klabu’ ya #MachesterCity, #KelvinDeBruyne ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofikisha mabao 100 kwenye ‘klabu’ hiyo baada ya kufunga mabao mawili kati ya manne siku ya Jana.

De Bruyne amefikia rekodi hiyo baada ya ‘mechi’ 372 akiwa Man City huku akifikisha ‘asisti’ 167 katika ‘mechi’ hiyo dhidi ya #CrystalPalace  iliyochezwa kwenye uwanja wa #SelhurstPark nchini Uingereza ambapo  mchezo ulimalizika kwa ‘klabu’ hiyo kupata ushindi wa mabao 4-2.

Mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2025 alijiunga ‘klabuni’ hapo mwaka 2015 akitokea ‘klabu’ ya #VfLWolfsburg iliyopo chini Ujerumani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags