Dayoo: Niliwahi kutapeliwa, Nipo tayari kujiunga na lebo yoyote kwa mashariti

Dayoo: Niliwahi kutapeliwa, Nipo tayari kujiunga na lebo yoyote kwa mashariti

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Dayoo, amedai kuwa yupo tayari kujiunga na ‘lebo’ yoyote ya muziki, lakini kwa mashariti ya kuzingatia uwekezaji uwe mkubwa huku hata baada ya kuachana na lable hiyo waendelee kuwa familia na sio kuchukiana.

Hata hivyo msanii huyo ameeleza kuwa wakati wa ku-shoot video anachukizwa na tabia ya baadhi ya ma-director kupenda kurahisisha mambo  bila kuzingatia uhalisia, huku akidai kuwa video yake ya Handsome ndiyo imetumia pesa nyingi zaidi ya zote alizowahi kufanya.

Aidha msanii huyo ameweka wazi ili aweze kufanya show na mtu kwa Tanzania analipisha kuanzia tsh 3 milioni, na akakumbushia kuwa wakati anajitafuta aliwahi kutapeliwa hela kwa kutolipwa baada ya kumaliza show.

Huku kwenye upande wa kuwalipisha wasanii wengine katika kufanya nao ngoma msanii huyo ameweka wazi kuwa halipishi kiasi chochote cha pesa labda msanii atake mwenyewe kulipa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags