Davis akamatwa kuhusishwa na kifo cha Tupac

Davis akamatwa kuhusishwa na kifo cha Tupac

Duane ‘Keefe D’ Davis ambaye alikuwa shahidi katika mauaji ya rapper Tupac Shakur, amekamatwa na ‘polisi’ akihusishwa moja kwa moja na mauaji ya msanii huyo aliyepigwa risasi katika mitaa ya Las Vegas nchini humo mnamo mwaka 1996.

Davis atasomewa mashtaka baada ya kudaiwa kuhusika na kifo cha msanii huyo licha ya mashtaka yake kutowekwa wazi.

Mwanzo Davis kufuatia ushahidi wake alisema alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari ya Cadillac nyeupe iliyokuwa na muuaji wa Tupac kisha akachukua bunduki iliyotumika katika mauaji hayo na kuirusha kuelekeza kwenye kiti cha nyuma, ambapo amesema ndipo risasi zilipofyatuliwa.

Tupac alikuwa kwenye gari aina ya BMW na alishambuliwa na risasi kadhaa na kupelekea kifo chake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags