Davido: Nilistahili kuwa na tuzo 20 za Grammy

Davido: Nilistahili kuwa na tuzo 20 za Grammy

Mkali wa #Afrobeat kutoka nchini Nigeria Davido amesema kuwa mpaka alipofikia alistahili kuwa na Tuzo 20 za #Grammy kutokana na ngoma zake kupigwa nchi tofauti tofauti.

Davido ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na kituo cha runinga cha ‘Farance 24’ baada ya kuulizwa swali kuhusiana na kutanjwa kwake kuwania Tuzo za Grammy kuna maana gani?, ndipo alieleza kuwa alifanya kazi kubwa kwenye albumu ya ‘Timeless’ hivyo alistahili kupata Tuzo za Grammy 20 hapo nyuma kama angeitoa mapema.

Ikumbukwe kuwa Davido ametajwa kuwania vipengele vitatu katika Tuzo za Grammy vikiwemo Best Global Music Album (Timeless), Best Global Music Performance (Feel, Unavailable), Best African Music Performance.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili Februari 4 katika ukumbi wa ‘Crypto.com Arena’ ulioko Los Angeles nchini Marekani.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Davido kuwania tuzo za Grammy, endapo atashinda atakuwa msanii wa pili kunyakua tuzo hizo, kwa sababu Wizkid ndiye msanii pekee wa Afrika ambaye amewahi kushinda Grammy mwaka 2020, katika kipengele cha ‘Video bora ya muziki’ kwenye ngoma aliyoshirikishwa na Beyonce ‘Skin Girl’.

Tuzo ya pili ya Grammy WizKid alichukua mwaka 2022 katika kipengele cha ‘Favorite Afrobeats Artist’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags