Davido kushughulika na wanaomfanyia ubaya

Davido kushughulika na wanaomfanyia ubaya

Mkali wa afrobeat kutoka nchini Nigeria Davido ameweka wazi kuwa sasa ataanza kushughulika na kulipiza kisasi kwa wale wote ambao wamewahi kumfanyia ubaya.

Davido kupitia ukurasa wake wa X (zamani twitter) amendika kuwa mtu yoyote ambaye amewahi kumfanyia ubaya wowote mwaka huu atalipa mmoja baada ya mwingine huku akidai kuwa ameanza sasa kulipa ubaya huo.

Aidha kupitia kauli hiyo iliyotelewa na Davido wadau mbalimbali walijitokeza katika upande wa ‘komenti’ wakimtaka msanii huyo aanze na Wizkid, kutokana na wawili hao kuingia katika bifu zito mwezi mmoja uliyopita na kupelekea kurushiana maneno kupitia mitandao ya kijamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags