Davido Kama Harmonize

Davido Kama Harmonize


Mkali wa afrobeat kutoka Nigeria Davido ameweka wazi kuwa ana mpango wa kuacha kuimba muziki.

Davido kupitia instastory yake ameeleza kuwa kuna watu hawamtakii mema wanataka aachane na game (muziki) hivyo basi baada ya kutoa album yake inayofuata atapumzika ili watu hao wawe na Amani.

Kufuatiwa na ujumbe huo baadhi ya mashabiki wamedai kuwa huwenda mwanamuziki huyo anataka kuacha muziki kutokana na ugomvi wake na msanii mwenziye Wizkid.

Davido siyo msanii pekee ambaye anampango wa kuachana na game ya mziki kwani wiki kadhaa zilizopita mwanamuziki nchini Tanzania Harmonize alidai kuwa anataka kuwekeza nguvu kwenye ndondi kwani kwenye tasnia ya muziki kumejaa chuki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags