Davido, Chioma Kufanya White Wedding Miami

Davido, Chioma Kufanya White Wedding Miami

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Davido ametangaza kufanya harusi nyingine ya ‘White Wedding’ jijini Miami nchini Marekan mwezi Agosti mwaka huu.

Davido ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha ‘The Break Fast Club’ ambapo ameweka wazi kuwa harusi yake aliyofanya 2024 ilikuwa ya kitamaduni hivyo amepanga kufanya balaa lingine la ‘White Wedding’ mwaka huu.

“Ile harusi ya Nigeria ilikuwa ya kutambulisha familia na kukutana pamoja, hivyo ntafanya White Wedding Miami, Marekani mwezi wa nane mwaka huu,”amesema Davido.

Aidha ameleza kuwa anafanya hivyo kwa sababu mke wake amekuwa bora zaidi na amemvumilia kwenye kila nyakati.

“Kwa sababu mimi na mke wangu mahusiano yetu yamekuwa hadharani, na ninachompendea mke wangu huwezi muona anaenda kwenye mahojiana kulalamika kuhusu mimi, au kuchukua simu yake kuingia live namkubali sana kwa sababu yuko poa, unajua hakuna aliekamilika tunapitia mengi,”amesema Davido

Hata hivyo, mashabiki wa muziki tokea nchini wametafsiri maamuzi hayo ya Davido kama sehemu ya kutaka kuifunika harusi ya msanii wa Bongo Fleva, Jux na mrembo Priscilla baada ya kutikisa mitandao ya kijamii huku ikitajwa kama moja ya harusi bora Afrika 2025.

Lakini ukweli ni kwamba Davido alifanya mahojiano hayo na kuweka wazi taarifa hiyo wiki mbili nyuma kabla ya harusi ya Jux na Priscilla hivyo ni mpango aliokuwa nao muda mrefu kabla ya harusi Ya Jux kutisa mitandao ya kijamii Afrika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags