Davido afunguka kwa mara ya kwanza kifo cha mwanae

Davido afunguka kwa mara ya kwanza kifo cha mwanae

Wote tunafahamu tokea itokee kifo cha mtoto wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria, David Adekele maarufu Davido hakuwahi kuzungumza chochote kinachohusu mtoto wake.

Lakini hivi karibuni amejitokeza na kusema kwamba anaendelea kumuomboleza mwanae kila siku.

Davido alizungumza na moja ya chombo cha habari anasema kwamba haikuwa rahisi kwake yeye kutoa albamu kwa jina Timeless baada ya kifo cha mwanawe

Kulingana na mahojiano hayo mashabiki wake wengi walitarajia kwamba angetunga wimbo wa huzuni katika albamu hiyo lakini badala yake aliamua kutunga wimbo ambao ungewafurahisha badala ya kuomboleza anasema.

“hakuna siku hata moja nimekaa bila kutoa machozi tangu kifo cha mwanangu lakini watu hawajui hilo”alisema mwanamuziki huyo.

Aliongezea kusema kwamba anapojiangalia katika kioo anajua kuna watu wanaweka matumaini kwake.  

“Najua kwamba mwanangu ananitazama kutoka mbinguni, mbali na hilo mwanangu asingependa nimvunje moyo kwasababu ya mama yake, lazima niwe mwangalifu kutokana na wapenzi wangu wa muziki kote duniani’’alisema Davido.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags