Davido afichua kilichofanya atoe album ya timeless

Davido afichua kilichofanya atoe album ya timeless

Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido ameweka wazi kuwa kufanya albumu ya Timeless ilikuwa ni kwa ajili ya uponywaji ndani yake kufuatia kifo cha mtoto wake Ifeanyi kilichotokea mwaka 2022.

Davido kupitia mahojiano yake na Zane Lowe of Apple Music 1, aliweka wazi suala hulo huku akidai kuwa tukio hilo lilimfanya kutengeneza zaidi ya ngoma 28 za albumu hiyo kabla ya kuzichagua.

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa ana ngoma kali kuliko hata zilizopo kwenye albumu ya Timeless zaidi ya 60 ambazo hazijatoka hivyo basi hana wasiwasi kwa sasa kuhusu kutoa ngoma kali.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post