Mmmmmmmh! Kwahiyo mnataka kutufanyia mambo ya mzee wa buga, basi bwana kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba msaanii wa hip hop Darasa aburuzwa mahakamani baada ya kutotokea katika show yake jijini Mbeya
Mbeya .Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imepokea shauri la madai dhidi ya Msanii wa kizazi kipya Shariff Thabeet maarufu (darasa) na Daniel Mwailubi Mmiliki wa Mwailubi Lounge kwa madai ya kuvunja mkataba na kuwadanganya wananchi kufanya tamasha la beer Festive Season 28 lililotakiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu.
Shauri hilo limewasilishwa na Mwanasheria wa Kampuni Baistar Advocate ya Jijini Mbeya dhidi ya wateja wake Arnold Francis Kisheni na Seiph Mussa Wembe mbele ya Hakimu Mkazi Happiness Chuwa mnamo Agosti 24 mwaka huu.
Mbwilo ameliambia Mwananchi leo Jumatatu Agosti 29 ,2022 kuwa awali shauri hilo lilipowasilihwa Mahakama mdaiwa wa kwanza Danny Mwailubi amepatiwa nakala ya madai na kutakiwa kupeleka utetezi wake Mahakamani Septemba 5 mwaka huu huku msanii Shariff Thabeet (darasa) wakiendelea kumtafuta .
Amesema kutokana na hadha waliyoipata na usumbufu kwa wateja wake wamewasilisha madai ya fidi a Sh 71.4 Milioni ikiwa ni madai halisi huku 200 Milioni fidia ya madhara waliyoyapata
Mbwiro ameeleza kuwa mnamo Julai 29 mwaka huu walalamikaji wakiwa Mpanda Mkoa wa Katavi waliona tangazo kwenye akaunti za Instagram za wadaiwa wakitangaza kuwepo kwa tamasha la Beer Festival Season 28 .
Tangazo hilo ambalo liliambatana na picha ya msaanii ,Sharif Thabeet maarufu kama ''darasa'' kwa kiingilio cha 10,000 na beer ambalo lililotakiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu na badala yake kuvunja makubaliano baina ya wadaiwa na wateja kwa msanii hiyo kutopanda stejini kama ilivyokuwa makubaliano.
''Wateja wangu walisafiri kutoka Mkoa wa Katavi kuja kushuhudia tamasha hilo lakini walikaa mpaka alfajiri pasipo msanii kupanda stejini na wala Mmiliki wa Mwailubi Lounge kuwaeleza chochote ''amesema.
Amesema kuwa kutokana na madhara waliyopata wamefungua kesi ya madai ya Sh 71.4 Milioni kama madai halisi huku Sh 200 Milioni fidia ya madhara (General Damages) pamoja na kuwataka kuomba msamahausio na masharti na kulipa gharama za uendeshaji wa kesi Mahakamani.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Mkoa wa Mbeya ,Happiness Chuwa amepanga kusikilizwa kwa shauri hilo namba 25/2022 Septemba 5 mwaka huu huku wakimtaka mmiliki wa Mwailubi Lounge apeleke utetezi wake Mahakamani ikiwa ni pamoja na kumtafuta msanii wa Kizazi kipya maarufu kama Darasa.
Amewataka wasanii na waendesha matamasha wajue sheria haipo kimya kwani ipo na inalinda upande zote mbili kwa walioandaa na waliohudhuria .
Leave a Reply