Dame akubali kumaliza tofauti na Jay Z

Dame akubali kumaliza tofauti na Jay Z

Dame Dash ambaye alikuwa akishirikiana na Jay Z kuimiliki ‘lebo’ ya ‘Rock A Fella’,  ameweka wazi kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na Jay Z ili wamalize tofauti zao na kurudisha nguvu katika ‘lebo’ hiyo.

Kufuatia mahojiano yake na ‘The CEO Show’, Dash ameweka wazi kuwa ugomvi wake na Jay ulikuwa ni kumuweka mbali msanii huyo na watu wake wa karibu wanaomtumia vibaya huku aliweka wazi kuwa lengo lake lilikuwa  kumuokoa msanii huyo

Kufuatia mazungumzo hayo Dash amedai kuwa hana kinyongo na Jay Z na yupo tayari kufanya mazungumzo nae huku akieleza kinacho wakwamisha ni kuwa kwa sasa kila mtu yuko busy na mambo yake.

Awali Dame na Jay-Z walikuwa wakifanya kazi pamoja na baadaye waliingia kwenye mgogoro wa kibiashara uliofanya wawili hao kutengana huku Dash akaamua  kuisusa Rock-a-fella.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags