Daladala lagonga treni na kuuwa mtu mmoja

Daladala lagonga treni na kuuwa mtu mmoja

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa leo Mei 18, 2023 majira ya asubuhi imetokea ajali katika makutano ya reli na barabara eneo la Kamata iliyohusisha Gari la abiria lenye namba za usajili T710 DKJ linalofanya safari kati ya Machinga Complex na Kigamboni baada ya kugonga behewa la breki ya treni ya Deluxe lenye namba 8637.

Taarifa iliyotolewa na TRC imeeleza kuwa ajali hiyo imesababisha kifo cha mtu mmoja (mwanamke) huku majeruhi wakiwa ni 15 ambapo wanawake ni 10 na wanaume 5, Majeruhi wamefikishwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu na wanaendelea vema

Aidha TRC imewasihi madereva wa vyombo vya moto kuzingatia alama za usalama barabarani na kuwa makini ili kuepusha ajali katika makutano ya reli na barabara






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags