Daladala alilopanda Odinga lapata umaarufu

Daladala alilopanda Odinga lapata umaarufu

Waswahili wanasema mgeni njoo mwenyeji apone, msemo huu umesaidiki, kupitia kijana David Murage ambae amejipatia umaarufu kwa siku tu baada ya kumsafirisha kiongozi wa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga.

Kwa mujibu wa TUKO, Murage alisema wakati wa mahojiano kwamba simu yake imekuwa ikiita kila mara tangu alipomsafirisha Waziri Mkuu huyo wa zamani hadi katikati ya jiji la Nairobi (CBD) katika daladala yake.

Dereva huyo alieleza kwamba siku hiyo bado inabakia isiyo ya kawaida kwake, akiongeza kuwa alishangaa kumuendesha mwanasiasa muhimu hadi CBD, Murage alisema kuwa haikuwa sherehe rahisi kumsafirisha Raila katika daladala yako, akisema kuwa kuna gari chache ambazo zinaweza kuhesabiwa kuwa zimembeba kiongozi wa ODM.

Alimalizia kwa kueleza kuwa “Hata sikufikiria ilikuwa tu surprise tu, si kawaida kubeba mtu kama huyo najua ashawai kuingia kupada basi lakini ni kidogo sana, but naona kumbemba hadi town ni privilege hiyo” alisema Dereva huyo  






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags