Daktari ashitakiwa, Unyanyasaji wa kingono kwa wagonjwa waliozimia

Daktari ashitakiwa, Unyanyasaji wa kingono kwa wagonjwa waliozimia

Dk. Louis Kwong, ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Mifupa katika Kituo cha Matibabu cha Harbour-UCLA Torrance, California, ameshitakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia, tabia ya ubaguzi na unyanyasi wa kingono kwa wagonjwa wanaopoteza fahamu

Inadaiwa kuwa daktari huyo amekuwa na tabia ya kuwafanyia unyanyasaji wagonjwa ikiweo kuingiza kidole chake kwenye jeraha la mgonjwa lililokuwa kiunoni na kuwafanyia vitendo vya kingono wagonjwa waliopoteza fahamu katika chumba cha upasuaji.

Malalamiko hayo yaliibuliwa na madaktari watatu wa kike ambao ni Dkt. Haleh Badkoobehi, Dkt. Jennifer Hsu, na Dkt. Madonna Fernandez, ambao katika malalamiko yao pia walidai wote walikuwa wakishushwa vyeo kila walipolalamikia tabia ya Kwong huku wasimamizi wa hospitali hiyo wakiwa wanapuuza malalamiko yao kwa miaka mingi.

Dk. Louis Kwong  anadaiwa kufanya kazi katika hospitali hiyo tangu 1990.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags