Daftari lenye mistari ya Wayne kuuzwa sh 13 bilioni

Daftari lenye mistari ya Wayne kuuzwa sh 13 bilioni

Daftari (notebook) ya zamani ya mwananamuziki Lil Wayne aliyokuwa akiitumia kuandika nyimbo zake mbalimbali lipo sokoni kwa ajili ya kuuzwa.

Kwa mujibu wa Tmz imeeleza kuwa daftari hilo la Wayne alilokuwa akitumia kuandika mashairi yake toka mwaka 1990 sasa lipo sokoni na linauzwa dola 5 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 13 bilioni.

Hata hivyo tovuti ya Tmz imeweka wazi kuwa atakae fanikiwa kununua daftari hilo basi atakutana na mashairi ya wimbo wa We On Fire’ na ‘I Feel’ aliyoyaandika wakati yupo katika kundi la ‘Hot Boys’ akiwa na miaka 17.

Utakumbuka kuwa mwaka 2019 mwanaume mmoja alitaka kuliuza daftari hilo akidai kuwa aliliokoto, hata hivyo Lil Wayne alipinga lisiuzwe kwani ilikuwa ni mali yake na hatimaye alishinda kesi mahakamani na kukabidhiwa tena daftari hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags