Curry, Drummond waipaisha Brooklyn Nets NBA

Curry, Drummond waipaisha Brooklyn Nets NBA

Moja ya story huko mitandaoni ya wachezaji Seth Curry na Andre Drummond ambao wamesaidia kuipa ushindi wa kwanza Brooklyn Nets wa alama 109 kwa 85 dhidi ya timu ngumu ya Sacramento Kings.

Ushindi huo umepatikana alfajiri ya kuamkia leo Jumanne Februari 15, 2022 baada ya vichapo 11 mfululizo kwenye NBA.

Mchezo huo ni mchezo wa kwanza kwa wawili hao waliojiunga na Brooklyn Wiki iliyopita wakitokea Philadelphia 76ers na kuonesha kiwango kizuri ambapo Seth Curry amefunga alama 23, rebound 7 na Assist 5.

Andre Drummond amefunga alama 11, rebound 9 na Assist 4 alama ambazo zimeifanya Brooklyn kutoka kutoka nafasi ya 11 kupanda hadi nafasi ya nane ambapo wanawania kumaliza katika nafasi hizo ili wacheze NBA Playoffs.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags