Cr7: Nitakuwa na mama yangu kila wakati

Cr7: Nitakuwa na mama yangu kila wakati

 Mchezaji kutoka ‘klabu’ ya #Al-Nassr, Cristiano Ronaldo ameeleza sababu ya kutomjengea mama yake na badala yake anaishi naye licha ya kuwa na utajiri wakutosha.

Akizungumza katika maojiano na moja ya chombo cha habari gwiji huyo wa mpira  anasema mama yake alijitolea maisha yake kwake kwani aliwahi kulala na njaa ili yeye ale, kuna kipindi hawakuwa na pesa hata kidogo na mama yake aliwajibika kwa hilo mchana na usiku kama kijakazi kununulia vifaa vya CR7 ili awe mchezaji.

Aliendelea kueleza kuwa mafanikio yake yote ni kwa sababu ya mama yake kujitolea, CR7 ameahidi atakuwa karibu na mama yake siku zote na kila wakati.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags