CR7 kumlipa mkewe million 257 kila mwezi kama wataachana

CR7 kumlipa mkewe million 257 kila mwezi kama wataachana

Kama kawaida ya mitandao kuvimisha mambo basi bwana waja wameangukia pua kwa Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez kuwa wanakaribia kuachana, wawili hao wameonesha kuwa hawayumbishwi na fununu hizo na kuamua kusaini makubaliano ya kabla ya ndoa (prenuptial agreement) kuhusu umiliki wa mali zao iwapo ndoa hiyo itavunjika siku za usoni.

Katika makubaliano hayo, ikiwa wawili hao wataachana basi Georgina atakuwa mmiliki pekee wa nyumba ya familia yao huko Madrid na atakuwa akipokea dola 107,500 takribani milioni 257 za Kitanzania kwa mwezi katika maisha yake yote.

Mahusiano ya Ronaldo na Georgina yalianza zamani alipokuwa Real Madrid baada ya kukutana katika duka la Gucci na hivi sasa wawili hao kwa pamoja wana watoto 5.

Kati ya watoto hao wawili ni wamezaliwa na Georgina huku wengine watatu wakipatikana kwa njia ya surrogate (kupitia mtu mwingine). Yaani mwanamke kuzaa mtoto wa niaba ya mwingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags