Cr7 ashinda kesi dhidi ya Juventus

Cr7 ashinda kesi dhidi ya Juventus

Nyota wa soka duniani #CristianoRonaldo ameshinda kesi ya madai ya mshahara dhidi ya klabu yake ya zamani ya #Juventus.

Klabu hiyo inatakiwa kumlipa CR7 kiasi Sh26.9 bilioni kama fidia ya malipo ya mshahara wake kuanzia mwaka 2020 hadi 2021.

Septemba mwaka jana Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al-Nassr ya Saudia aliamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ‘klabu’ hiyo kwa kutolipwa mshahara wakati wa janga la Covid-19.

2020 ‘klabu’ hiyo ilikubaliana na wachezaji kukata mishara yao kwa sababu ya mlipuko wa Covid-19 na kuahidi watawalipa baada ya kipindi hicho kuisha.

Ronaldo alijiunga na miamba hiyo ya Italia mwaka 2018 ambapo aliisaidia timu hiyo kuchukua baadhi ya vikombe kabla ya kwenda #ManchesterUnited mwaka 2021.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BuruidikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags