Cr7 akataa ‘penati’ ya mchongo

Cr7 akataa ‘penati’ ya mchongo

Mchezaji wa 'klabu’ ya Al Nassr, #CristianoRonaldo amekataa ‘penati’ aliyokuwa amepewa na refa kwenye mchezo wa ‘klabu’ bingwa bara la #Asia siku ya jana, baada ya Ronaldo kuanguka ndani ya box na Refa kuonesha ni ‘penati’.

Inadaiwa kuwa CR7 alimfuata Refa aliyekuwa amezingirwa na baadhi ya nyota wa ‘klabu’ ya Persepolis na kumwambia siyo ‘penati’ hivyo Refa akaenda kujiridhisha kwenye VAR na akakubali kuwa haikuwa tuta.

Mchezo huo dhidi ya ‘klabu’ ya Persepolis na Al Nassr ulimalizika kwa ‘timu’ zote mbili bila kupata bao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags