Consolee Uwimana achaguliwa kuwa Naibu wa Kagame

Consolee Uwimana achaguliwa kuwa Naibu wa Kagame

Chama tawala nchini Rwanda, Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), jana jumapili kilimchagua mwanamke wake wa kwanza kuwa makamu mwenyekiti huku Rais Paul Kagame akishikilia nafasi ya uenyekiti ambapo alipata 99.8% ya kura zilizopigwa.

Consolee Uwimana alichaguliwa kwa kura 1,945  takriban 93% ya kura zilizopigwa, mwanamama huyo ambae alikuwa ni mfanyakazi wa benki kwa muda mrefu na mfanyabiashara ambaye alihudumu kama seneta kati ya 2003 na 2013.

Waangalizi wa mambo wanasema kumpandisha cheo ni njia ya chama kutoa mamlaka zaidi kwa wanawake na kuweka uwiano wa ukabila katika uongozi wake mkuu.

Ikimbukwe tu uchaguzi mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika mwaka 2024.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags