Chura mkubwa zaidi ambaye awali maafisa wa wanyama pori walifikiri ni bandia amepatikana katika msitu wa mvua kaskazini mwa Australia.
Chura huyo mwenye jina la “Toadzilla” anadaiwa kuwa mkubwa mara sita kuliko wa kawaida, ana uzito wa kilo 2.7 na anaweza kuvunja rekodi ya dunia.
Chura ambao waliletwa Australia kwa mara ya kwanza mnamo 1935 ni moja ya wadudu waharibifu zaidi nchini humo na sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 2.
Wakati mlinzi wa bustani hiyo ya Kylee Gray alipomwona mnyama huyo mkubwa kwa mara ya kwanza akiwa kwenye doria huko Queensland, hakuamini macho yake.
"Sijawahi kuona chura mkubwa hivyo, alionekana kama mpira wa kandanda wenye miguu, tulimuita Toadzilla," aliambia Shirika la Utangazaji la Australia.
Rekodi ya sasa ya dunia ya Guinness kwa chura mkubwa zaidi ni uzito wa 2.65kg iliyowekwa na chura wa Uswidi aitwaye Prinsen mnamo 1991.
Bi Gray anasema spishi hii kubwa inaweza kuwa iliacha kula lishe ya kawaida ya wadudu, wanyama watambaao na mamalia wadogo.
"Chura wa ukubwa huo atakula chochote kinachoweza kutoshea mdomoni mwake," alisema.
Leave a Reply