Chuo kikuu Uganda chapiga marufuku kamera katika mahafali

Chuo kikuu Uganda chapiga marufuku kamera katika mahafali

Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kimepiga marufuku wanaohudhuria sherehe za kuhitimu kubeba simu, kamera za video, kwa mujibu wa taarifa.

Chuo hicho kitafanya sherehe leo Jumatatu ya kuhitimu ya siku tano kwenye Uwanja wake wa Freedom Square. Jumla ya wanafunzi 13,221 wamepangwa kuhitimu, huku kila mmoja akiruhusiwa kualika wageni wawili pekee.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kupigwa marufuku kwa kamera katika uwanja wa mahafali, lakini vitu vingine vilivyopigwa marufuku kwenye sherehe hiyo ni pamoja na pombe, sigara, vyakula vya makopo na vinywaji vya chupa.

“Orodha ya kina ya bidhaa zilizopigwa marufuku imeingizwa kwenye kifurushi cha mialiko ya kuhitimu ambayo huwasilishwa kwa wahitimu na wageni waalikwa," mkuu wa kamati ya sherehe, Prof Patrick Mangeni, alisema

Mke wa Rais Janet Museveni, ambaye pia ni waziri wa elimu ya msingi, anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags