Chris Brown ampa maua yake Tina Davis

Chris Brown ampa maua yake Tina Davis

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Chris Brown amerudisha fadhila kwa mmiliki wa kampuni ya kurekodi na usambazaji muziki ya Empire, Tina Davis kwa kumpa maua yake mwanamama huyo akimtaja kuwa ni moja ya mtu aliyechangia kujulikana zaidi.

Brown ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na podicast ya ‘R&B Money’ ambapo alikumbuka mchango wake kwake huku akimtaja Tina kuwa ni mtu powa sana.

Tina Davis ni Rais wa Empire kampuni huru ya kurekodi, usambazaji na uchapishaji pia aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza idara ya A&R katika Def Jam, hapo awali alianza kazi kama makeup artist akitumia fani hiyo kwa wasanii wakubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags