Chris Brown amfagilia Wizkid

Chris Brown amfagilia Wizkid

Msanii kutokea nchini Marekani Chris Brown ameonesha kufurahishwa na hatua ambazo anaendelea kuzipiga msanii kutokea pande za Nigeria Wizkid katika muziki wake.

Usiku wa kuamkia jana, Wizkid alifanya show huko Uingereza katika ukumbi wa 02Arena, na kumpandisha msanii Chris Brown kisha kushare naye stage katika ukumbi huo.

Baada ya show, masaa machache yaliyopita Chris Brown ametumia ukurasa wake wa Instagram kumwagia sifa Wizkid na kumshukuru kwa kumpandisha kwenye stage hiyo, huku akieleza kuwa wawili hao wamekuwa marafiki kwa takribani miaka 10 sasa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags