Chris aliwahi kumuomba  Jada watoke, baada ya kusikia kaachana na Smith

Chris aliwahi kumuomba Jada watoke, baada ya kusikia kaachana na Smith

Jada Smith ambaye aliyekuwa mke wa muigizaji Will Smith, amefichua kuwa Chris Rock aliwahi kumuomba watoke baada ya kusikia ameacha na Will.

Jada akiwa kwenye mahojiano na jarida la People wakati akitangaza kitabu chake ameeleza kuwa mwaka 2016 zilivuma tetesi za yeye kuachana na Will Smith, na zikapelekea apokea simu kutoka kwa mchekeshaji Chris Rock akimuomba waende mtoko.

Kutokana na ombi hilo Jada ameeleza kuwa ilibidi amuuliza Chris anacho maanisha lakini mchekeshaji huyo alimjibu kwa kuwa ameachana na Will basi anaomba nafasi ya kutoka naye, Jada amedai alimueleza Chris kuwa taarifa hizo hazina ukweli ndipo mchekeshaji huyo aliomba msamaha.

Hata hivyo Jada hakuacha kuzungumzia tukio la Will Smith kumpiga kofi Chris Rock kwenye usiku wa tuzo za Oscar 2022, huku akidai kuwa kwa upande wake alihisi kama tukio hilo halikuwa la kweli hadi alipoona Will anarudi kukaa kwenye kiti ndipo aliamini alichokiona na kupelekea amuulize Will kama yupo sawa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags