Chidimma ajiondoa kwenye mashindano ya Miss S.A

Chidimma ajiondoa kwenye mashindano ya Miss S.A

Baada ya kuzuka tetesi kuwa mwanamitindo Chidimma Adetshina (23) anayeshiriki ‘Miss Afrika Kusini’ kubaguliwa kwenye shindano, kwa madai ya kuwa ni raia wa Nigeria hatimaye mwanadada huyo ameamua kujiondoa kwenye shindano hilo ikiwa ni siku chache tu kuelekea fainali.

Chidimma ameweka wazi kuwa alitamani kuendelea kushiriki katika shindano hilo lakini anaamua kujiondoa kwa ajili ya usalama wa familia yake.

“Kuwa sehemu ya shindano la Miss Afrika Kusini 2024 imekuwa safari ya kuvutia sana, hata hivyo, baada ya kutafakari kwa kina, nimechukua uamuzi mgumu wa kujiondoa katika mashindano hayo kwa ajili ya usalama na ustawi wa familia yangu na mimi mwenyewe,"ameeleza



Utakumbuka kuwa siku chache zilizopita mitandao ya kijamii ya Afrika Kusini ilizua mijadala kuwa mmoja wa washiriki katika mashindano hayo siyo mtu wa taifa hilo wakidai kuwa ni Mnigeria huku wakihofia mrembo huyo kuwa huenda akaibuka mshindi kwenye fainali ya Miss SA zinazotarajia kufanyika Agosti 10, 2024.

Ukiachilia mbali minong’ono hiyo waandaaji wa shindao la ya ‘Miss South Africa’ walilitolea ufafanuzi suala hilo na kuweka wazi kuwa Chidima ni raia wa nchi hiyo na alizaliwa Soweto na kukulia Cape Town hivyo anahaki ya kushiriki mashindano hayo.

"Chidima alizaliwa na kukulia katika kitongoji cha Soweto, Gauteng huku baba yake akiwa ni Mnigeria na mama akitambulika kama raia wa Afrika Kusini, kwa maelezo haya yanamfanya mrembo huyo kuwa na uraia wa nchi mbili," imeeleza taarifa iliyotolewa na waandaaji wa Miss SA






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags