Chidimma afunguka baada ya kushinda taji Miss Universe Nigeria

Chidimma afunguka baada ya kushinda taji Miss Universe Nigeria

Mwanamitindo Chidimma Adetshina amefunguka ya moyoni baada ya kushinda taji la ‘Miss Universe Nigeria’ kwa kuwataka Waafrika kuacha kubaguana wenyewe kwa wenyewe.

Chidimma ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kutoa shukrani kwa jamii na wote waliomuunga mkono katika safari yake pamoja na kuwaonya wadau mbalimbali kuvunja vikwazo vinavyowatenganisha watu.

“Ninapokubali heshima hii, nataka kushiriki maono ambayo yanawaka ndani yangu, maono ya umoja wa Afrika na kuishi kwa Amani. Tuvunje vikwazo vinavyotutenganisha. Tuunde bara ambalo kila Mwafrika anaweza kusafiri kwa uhuru bila ubaguzi, kufuatilia ndoto zao na kuchangia katika ukuaji na ustawi wa bara letu kubwa.

"Taji hili siyo tu ishara ya uzuri, bali ni wito wa kuchukua hatua. Asanteni nyote kwa msaada na imani yenu kwangu. Ninahamu kubwa ya safari ijayo na nafasi ya kutumikia kama Miss Universe Nigeria. Shukrani za pekee kwa familia yangu ambayo imekuwa nami katika kila changamoto, kila machozi, na kila ushindi, hii ni kwa ajili yenu. Upendo na msaada wenu umekuwa msingi wangu.

"Shukrani za pekee kwa marafiki zangu na mashabiki ulimwenguni kote Mungu na ibariki Nigeria, Mungu na ibariki Afrika, na Mungu abariki kila mmoja wenu” ameandika Chidimma.

Ikumbukwe kuwa awali mrembo huyo alishindania taji Miss Afrika Kusini na mapema mwezi Agosti wananchi wa Afrika Kusini walikataa Chidimma kushiriki taji hilo kwa kudai ya kuwa mrembo huyo ni raia wa Nigeria.

Hata hivyo, baada ya minong’ono hiyo Chidimma aliamua kujitoa katika mashindano hayo kwa lengo la kulinda usalama wake na wa familia yake. Baada ya hapo aliibuka tena Nigeria na ndipo ameondoka na taji la ‘Miss Universe Nigeria’ ambapo atakwenda kuiwakilisha nchi hiyo kwenye shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Mexico Novemba 2024.

Chidima alizaliwa na kukulia katika Kitongoji cha Soweto, Gauteng huku baba yake akiwa ni Mnigeria na mama akitambulika kama raia wa Afrika Kusini, kwa maelezo haya yanamfanya mrembo huyo kuwa na uraia wa nchi mbili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post