Chidi Beenz aziamisha upya hisia za mashabiki

Chidi Beenz aziamisha upya hisia za mashabiki

Baada ya kionjo cha wimbo kati ya Diamond na Chidi Beenz kusikika siku chache zilizopita, imeonekana wadau wengi wa muziki walikuwa na hamu ya kusikia tena sauti ya Chidi  ambayo haijasikika kwa muda mrefu.

Wengi wamempokea kwa mapenzi makubwa mkali huyo, kwani katika mitandao mbalimbali ya kijamii kila mmoja amekuwa akizungumzia lake juu ya ujio wa Chidi huku wengine wakisubiri kwa hamu ngoma yake.

Kwa upande wa maoni pia yamekuwa yakitolewa mengi kwa kudai kuwa kufanya kwake ngoma na Diamond ndiyo mwanzo mpya wa kurudi kwake kwenye game.

Chidi wengi walimfahamu na kumpenda kwa ngoma zake mbalimbali kama vile “Mashallah”, “Nalia”, “Blood” na nyingine nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags