Chid Benz: Wameniibia fedha zangu, Mimi sio kichaa

Chid Benz: Wameniibia fedha zangu, Mimi sio kichaa

Msanii wa muziki nchini ambaye aishiwi na vituko, Rashid Mohamed maarufu kama Chid Benz amedai kuibiwa fedha zake na yupo tayari kuweka wazi ni kina nani wanafanya mambo hayo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii rapa huyo mkongwe wa Bongo Flea ameandika kuwa:

“Kuna namna Wasanii wanakua chini kifedha but saa zingine kuna mengi. Kuna wengi ambao wanasababisha maisha hayo na wao hawaonekani wala kujulikana zaidi ya wao tena kuchangia uonekane umefeli.

“Kuna namna nimefatilia pesa zangu na watu wanaozimiliki na kuziiba. Okke kuna wakati Binadamu unaghafilika ila haimaanishi uchukue vyangu kwa ujinga unauona wewe.

Nimepigania nchi yangu nimepigania mashabiki wangu na nimewapa burudani wananchi wangu wa ndani na nje. Bora kuniibia au kunionyesha labda sitokula mimi ila wanangu watapata na mama zao? familia yangu pia hata mashabiki zangu,” ameandika na kuongeza

“Unaiba zangu za wengine na husaidii chochote zaidi ya kubomoa kuhonga na kula Bata. Then mimi kichaa?? Okkay. Online tvs watu wa habari na vyombo vyote kwa faida ya kizazi kijacho namba hii hapa. NATAKA KUONGEA. 0764155608″,” amesema

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags