Chanzo na Dalili za upungufu wa Nguvu za Kiume

Chanzo na Dalili za upungufu wa Nguvu za Kiume

Hellowo! It’s anather furahi day mtu wangu wa nguvu, kama kawaida yetu week hii nina nyie siwezi acha ongea na nyie labda mje mniue, hahhaha! Jokes, sasa leo nimekuja na ile mada konki kabisa inayosababisha wanaume wengi kupoteza nguvu za kiume.


Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;


Baadhi ya vyanzo vya kukosa/upungufu wa nguvu za kiume

  1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
  2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe
  3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
  4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  5. Kisukari
  6. Kuwa na mawazo na wasiwasi
  7. Matumizi ya madawa mbalimbali
  8. Umri hasa wazee
  9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili, mfano dado kiki, konyaji nk
  10. Kuwa na tatizo la kibofu
  11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu
  12. Kutopata usingizi kamili, ndo mana tunashauliwa kulala walau masaa 8 kwa siku ili kupumzisha mwili
  13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine.

Dalili za upungufu wa nguvu za kiume

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;

  1. Kuwahi kufika kileleni
  2. Kukosa hamu ya mapenzi
  3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa, yani unakwenda raundi moja tu na kujihisi uchovu na kutotamani kurudia tena.
  4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha
  5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji
  6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo, ieleweke kuwa sio mwanamke peke yake huwa anapata maumivu bali hadi mwanaume pia na hii hutokea pale tu nguvu kupungua makali.
  7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)
  8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags