Changamoto wanazo kumbana nazo wauzaji wa simu

Changamoto wanazo kumbana nazo wauzaji wa simu

Hellow! I hope mko pouwa watu wangu  wa nguvu, tualikane basi hayo mabiriani sio mle wenyewe, au ndo mpaka tuongee kiarabu hahahah! (Jokes), kama kawaida katika kulizongesha gurudumu letu na kukufanya wewe msomaji wetu unapata kile ukitakacho.

Sasa leo katika segment yetu ya biashara tunakusogezea biashara ambayo ina changamoto nyingi sana na watu wengi ni ngumu kuwaamini kutokana na matapeli baadhi kuwaharibia wenzao biashara.

Embu nikuulize hivi ukitaka kununua simu wewe unaenda kununulia wapi? Najua wengi watasema kkoo, sinza or mlimani city, lakini ukitaja sehemu inayoitwa makumbusho basi kila mtu atashtuka na kuona kama unatapeliwa.

Kama tunavyojua wauzaji wengi wa simu makumbusho biashara yao imekuwa hatiani kufuatia watu wale wachache ambao wanaharibu biashara hiyo, kama kawaida yetu jarida la mwanamchi scoop moja kwa moja mpaka makumbusho na kuwakamata wauzaji wawili watueleze je yanayosemekana katika mitandao ya kijamii ni kweli kuwa wao ni matapeli.

Linus Gelase ni mfanyabiashara wa kitambo kidogo ambapo baishara hii alianzia akiwa chuo kwa kushirikiana na marafiki zake ambao tayari wako na maduka kwa kuwauzia simu wanafunzi wenzie chuoni.

Punde si punde alifanikiwa nayeye kufungua duka lake, ambalo alilipa jiana la Furahisha Electronics lililoko makumbusho bus stand, licha ya kuwa na changamoto nyingi katika mazingira hayo lakini hakukata tamaa hivyo basi alisonga mbele.

Basi bwana leo ameamua kufunguka kuhusiana na changamoto wananzokumbana nazo baadhi ya wauzaji wa zimu.

“Changamoto kuwa ni uaminifu wauzaji wa simu makumbusho tuna sifa mbaya sana mpaka mteja akuamini ni nguvu ya ziada inatumika so kwangu mimi hiyo ndo changamoto kubwa yaani natumia ngumu kubwa mno kuwashawishi wateja” amesema Linus Furahisha

Mbali na changamoto hiyo kubwa kuna nyingine ambazo zinawarudisha nyuma alifunguka na kueleza kuwa “Changamoto nyinyine ni utapeli unaenda kufanya deliver kumbe sio mteja ni wezi wanakupora simu na wanaweza kukuumiza pia” amesema Furahisha

Aidha alimalizia kwa kusema kuwa “Restrictions kwa mfano kutoa simu china ni changamoto kwa sababu bado hawaruhusu watu kuingia kutoka na magonjwa, Transportation ya simu wanakata kodi kubwa siku hizi na kubwa kuliko ni wauzaji wa simu kuwa wengi wengine wanauza used kama mpya, wanauza at lower price kwa sababu walichukua bei ndogo, so nawashauri wanaotaka kununua simu wawe makini san asana” amesema Linus Gelase

Hatukuishia hapo moja kwa moja safari yetu tukaibuka kwa mfanyabiashara mwingine ambaye yeye nae alitueleza kuhusiana na changamoto anazokumbana nazo katika biashara hii.

Noel Maskamo yeye kwa upande alieleza kuwa “ changamoto kubwa niniyakumbana nayo ni mabinti kujirahisisha waweze kupata simu za bure sasa hawajui kuwa wanaturudisha nyuma maana mtu unampunguzia lakini bado tu so hi indo changamoto kubwa nafikiri inatupa wauzaji wa simu wengi” amesema Noel

Mwamba huyo bwana leo ameamua kuongea ukweli japo kuna baadhi ya wauzaji wanasitasita kuliongea hili swala, aliendelea kwa kusema kuwa “ changamoto ni zile zile kuletewa simu fake, au simu ambazo haujaziagiza na kuibiowa wa watu unaokwenda kuwafanyia deliver” amesema Maskamo

Haya haya! Jamani jamani wadada mpunguze kidogo wenzenu wanafamilia, hizo biashara ndo wanatumia kuendeleza maisha yao yote, I hope leo tumejifunza kitu kwa wale wote wanaotaka kufanya biashara hii hizi ndo baadhi tu ya changamoto so kama unataka kuifanya ifanye tuu kwa moyo mmoja usiangalie changamoto zake.

Tukutane tena katika jarida lijaro bye bye!!!

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post