Changalawe apoteza pambano

Changalawe apoteza pambano

Bondia kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni nahodha wa ‘timu’ ya taifa ya ngumi, Yusuf Changalawe amepoteza pambano lake la ‘fainali’ ya kuwania ‘tiketi’ ya kucheza michezo ya Olimpiki mwakani Jijini Paris, nchini Ufaransa baada ya kushindwa kwa point dhidi ya Abdelrahman Abdelgawwad kutoka Misri.

Licha ya bondia huyo kupoteza ameshinda medali ya fedha pia anaweza kubahatika kupata nafasi ya upendeleo kushiriki mashindano hayo mwakani.

Aidha mabondia wengine watano wa Tanzania walitolewa mapema wakiwa ni Abdallah Katoto na Grace Mwakamele walioishia robo fainali, Musa Maregesi na Zulfa Macho Yusufu walioishia 16 bora ni Muharami Mohamed aliyetolewa ‘raundi’ ya pili tu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post