Chama: Hakuna haja ya kunyoosheana vidole

Chama: Hakuna haja ya kunyoosheana vidole

Mchezaji wa ‘Klabu’ ya Simba Clatous Chota Chama ametoa ushauri kufuatia yanayo endelea katika ‘timu’ yake kwa kueleza kuwa kwa sasa haina haja ya wao kunyoosheana vidole ni kuangalia namna gani wanaweza kuipambania ‘klabu’ hiyo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Chama ameshusha ujumbe ukieleza kuwa katika hali kama hii haina haja ya kunyoosheana vidole na kuhamisha majukumu kwa watu wengine kwa sababu haita saidia chochote.

Huku akiendelea kwa kueleza kuwa sasa ni wakati muafaka wa ‘klabu’ hiyo kushikana mikono kuweka mioyo na vichwa pamoja. Hii inakuja baada ya kutokea sintofahamu katika ‘Klabu’ ya Simba baada ya kupokea kipiga cha bao 5-1 dhidi ya watani wao Yanga.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags