Celine Dion kutumbuiza olimpiki Paris 2024

Celine Dion kutumbuiza olimpiki Paris 2024

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Canada, Celine Dion ameripotiwa kutumbuiza  katika sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 licha ya kuwa na ugonjwa wa Stiff Person Syndrome (SPS).

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zimeeleza kuwa michezo ya Olimpiki inatarajia kuanza Ijumaa, Julai 26 mwaka huu na kumalizika Agosti 11, 2024, jijini Paris, Ufaransa.

Aidha waimbaji wengine wanaotarajia kutumbuiza katika sherehe ya michezo hiyo ni pamoja na Dua Lipa kutoka Albanian na Aya Nakamura kutokea Paris.

Tovuti ya Sky Sport News inaeleza kuwa katika mashindano hayo yanakadiriwa kuwa na watazamaji zaidi ya 600,000 na yataoneshwa kwenye ‘skrini’ kubwa 80 katika maeneo ya umma.

Utakumbuka kuwa June mwaka huu msanii huyo mwenye umri wa miaka 56 alifunguka namna ambavyo alificha ugonjwa unaomsumbua licha ya kuwa dalili zake alianza kuziona mwaka 2008.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post