Cardi B athibitisha kuwa ujauzito ni wa Offset

Cardi B athibitisha kuwa ujauzito ni wa Offset

Baada ya kuwepo na minong’ono kupitia mitandao ya kijamii ambayo baadhi ya mashabiki wakitaka kujua ujauzito aliyonao Cardi B ni wanani, sasa msanii huyo ameweka wazi kuwa ujauzito huo ni wa baba watoto wake Offset.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani za kudai talaka Cardi aliwekawazi kuwa ujauzito alioubeba ni wa Offset hivyo basi suala hilo haliwezi kumfanya asiendelee na mchakato wa talaka.

Hata hivyo mwanamuziki huyo pia alifunguka kuwa anachokihitaji kutoka kwa Offset ni huduma za watoto wao watatu tu na sio kuwa naye kwenye mahusiano tena.

Utakumbukwa kuwa kabla ya Cardi B kutangaza kuwa ni mjamzito Tmz ililiripoti kwamba‘rapa’ huyo amefungua shauri Mahakamani akidai talaka, hii ni baada ya kusambaa kwa picha za Offset mitandaoni zikimuonesha akiwa kwenye huba zito na mpenzi wake wa zamani.

Hii sio mara ya kwanza kwa Cardi kudai talaka kwani mwishoni mwa mwaka jana alidai talaka lakini baada ya mwezi mmoja kupita wawili hao walirudiana tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags