Cardi B ajifunza kwa Beyonce kupuuza wanaomsema vibaya mitandaoni

Cardi B ajifunza kwa Beyonce kupuuza wanaomsema vibaya mitandaoni

Rapper Cardi B ameweka wazi kuwa hatoshughulika tena na watu wanaomsema vibaya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo.

Cardi B ameyasema hayo akiwa kwenye podcast ya “The Spout”, ambapo amedai kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Beyonce hasa katika kumuacha kila mtu aseme analotaka bila yeye kuingilia kama alivyokuwa akijibizana mwanzo na watu kwenye mitandao ya kijamii.

Amedai kuwa amejifunza kwenye kukaa kimya kutamsaidia hasa katika kuimarisha afya yake ya akili kwani kila mtu huwa na lake kwenye mitandao ya kijamii hivyo basi kwa sasa hatowajibu tena kwani analinda afya yake ya akili.

Ilizoeleka Cardi B alikuwa na kawaida ya kujibizana na mashabiki wanaomsema vibaya kwenye mitandao ya kijamii na alifikia hadi hatua ya kumshitaki shabiki mmoja aliyemzushia mume wake kuwa anamchepuko, lakini kupitia Beyonce anadai hatojibizana tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags