Cardi B adai kufunguka kuhusu maisha yake na Offset 2024

Cardi B adai kufunguka kuhusu maisha yake na Offset 2024

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani, #CardiB adai kufunguka kuhusu maisha yake ifikapo mwaka 2024, baada yeye na mumewe Offset kutofautiana na kufutiana urafiki Instagram, huku akidai anataka kuanza mwaka mpya akiwa huru.

Mshindi huyu wa Grammy mwenye miaka 31, ameahidi kueleza hayo akidai kuwa itakuwa ni faida kwa watu wengi wanaolinda vitu vinavyowatesa kwa sababu ya hisia za watu wengine.

Offset na Cardi B walifunga ndoa mwaka 2017 na wamefanikiwa kupata watoto wawili Kulture Kiari Cephus mwenye umri wa miaka mitano na Wave Set Cephus mwenye miaka miwili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags