Cancelo kutimukia Barcelona

Cancelo kutimukia Barcelona

Mchezaji wa Manchester City, Joao Cancelo, inadaiwa kuwa yuko mbioni kuondoka katika ‘klabu’ yake ya sababu kwa madai ya kutopata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha ‘timu’ hiyo, msimu huu akiwa hajacheza hata mechi moja.

Ingawa msimu uliyopita alicheza kwa mkopo kwenye team ya  #BayernMunich ambayo haikuonekana kushawishika kumsajili mazima licha ya kucheza ‘mechi’ 21 za michuano yote.

Licha ya hayo kuna taarifa za beki huyo kuwa anatarajiwa kuwasili jijini Barcelona kukamilisha uhamisho katika dirisha la msimu huu na kudaiwa kuwa wakala wake Jorge Mendes atakutana na ‘mabosi’ wa #Barcelona kwa lengo la kujadili dili hilo.

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags