Kufuatia tukio la zaidi ya watu 100 kufariki katika sherehe ya harusi na wengine zaidi ya 150 baada ya moto kuwaka kwenye ukumbi wa harusi hiyo, katika wilaya ya Al-Hamdaniya nchini Iraq, bwana harusi azungumza kwa mara ya kwanza tangu tukio hilo litokee.
Kupitia mahojiano yake na Sky news bwana harusi ameeleza kuwa mkewe amepoteza ndugu zake 10 wa familia moja, jambo ambalo limempa mshituko na kumfanya asiongee chochote huku bwana harusi akiwa amepoteza watu 15.
Katika mahojiano hayo bwana harusi huyo anayeitwa Revan amesema,
“Ni kweli tumekaa mbele yako tukiwa hai lakini ndani tumekufa, miili imekufa ganzi, moto ulivyo tokea nilimshika mke wangu na kuanza kumburuza alishindwa kutembea kwa sababu ya mavazi yake, nilimburuza na kumtoa nje kupitia mlango wa jikoni.
Kwa nini hii ilitokea kwetu kwani tumefanya kosa gani, mfano mke wangu amepoteza ndugu kumi mama yake, kaka zake, hawezi kuongea toka tukio limetokea amepata majeraha katika miguu yake baada ya watu kumkanyaga kipindi wakikimbia ”
Pamoja na hayo Revan ameeleza kuwa yeye na mkewe Haneen hawatoweza kuishi katika mji huo kwa sababu baadhi ya watu wanawatazama tofauti.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply