Burna Boy kulipa blog ziache kuandika habari zake

Burna Boy kulipa blog ziache kuandika habari zake

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria Burna Boy ameweka wazi kuwa atalipa blog yoyote nchini humo, ili ziache kuandika story zinazo muhusu.

Kupitia ukurasa wake wa X ame-share ujumbe huo kwa kueleza kuwa hajawahi kulipa pesa kwa blog yoyote nchini Nigeria ili iandike story zake hivyo amezitaka blog mbalimbali ziache ku-post story zake na yuko radhi kuwalipa kiasi chochote cha pesa.

Burn Boy anaendelea kufanya vizuri katika muziki wa Afrobeat ambapo anatamba na ngoma zake kama ‘Last Last’ ‘For My Hand’ aliomshirikisha Ed Sheeran, ‘It's Plenty’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags