Burna Boy: Hakuna anayeweza kuandika wimbo wa hadhi yangu

Burna Boy: Hakuna anayeweza kuandika wimbo wa hadhi yangu

Mwanamuziki wa Nigeria, #BurnaBoy amedai kuwa hakuna mwandishi wa nyimbo anayeweza kuandika wimbo wa hadhi yake. 
Burna Boy ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa X (Zamani Twitter) ambapo ameandika kuwa jina lolote linaloonekana katika nyimbo zake kama Pruducer au msanii aliyemshirikisha hawezi kuwa mwandishi wake. 

Hata hivyo kupitia maandiko hayo ameleeza kuwa kuna muda mataifa ya Magharibi huweka watayarishaji kama waandishi wa beat na kuweka majina yao kwenye nyimbo kama waandishi huku akidai kwa upande wake hakuna anayeweza kuandika wimbo wa hadhi yake.  

Hayo ni baada ya msanii Logos Olori ambaye kwa sasa anamtungia nyimbo Davido, kudau kuwa siyo bosi wake tu anayetungiwa nyimbo bali  Wizkid, Burna Boy na wasanii wengine wakubwa wanatumia watunzi wa nyimbo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags