Burna Boy aweka wazi tofauti yake na Wizkid

Burna Boy aweka wazi tofauti yake na Wizkid

Hahahaha! Kivumbi leo bwana msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy amefunguka na kuweka wazi tofauti yake na msanii mwenzie Wizkid  kwenye game ya muziki.

Kwenye interview yake ya hivi karibuni ameeleza kuwa style yake ya muziki na Wizkid ni tofauti kabisa wala haziendani ila wanachofanana yeye na Wizkid wanapendana na wanatoka sehemu moja, Lakini muziki wa Wizkid ni kuhusu mapenzi/wanawake huku yeye akiimba kuhusu maisha halisi (Hustling).

Alooooh! Haya kujeni hapa ety nyie mashabiki wa mwamaba Burna Boy je ni hicho tu wanachotofautiana na Wizkid au kuna kingine, dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags