Burna Boy awashangaza watu katika shindano la kuonja wali

Burna Boy awashangaza watu katika shindano la kuonja wali

Msanii kutoka nchini Nigeria Burba Boy amewashangaza wengi baada ya kuweza kukisia aina za wali, kutoka mataifa mbalimbali katika challenge ya kutambua aina ya mchele na nchi uliyotoka.

Akiwa katika mahojiano na Complex, Burna Boy alipewa aina mbalimbali za wali kutoka nchi za kiafrika na kisha alitakiwa kuonja na kukisia mchele uliyopikiwa wali huo ni kutoka nchi gani, lakini katika hali ya kushangaza nyota huyo aliweza kukisia na kupatia aina zote alizopewa kasoro aina moja tu ndiyo alikosea.
Burna alipatia nchi zote na mchele ulipotoka kasoro mchele wa Ghana tu ndio alishindwa kutambua umetoka wapi na hata alipo ambiwa ni mchele kutoka Ghana mkali huyo wa muziki alionesha kushangaa na kisha kuusifia kuwa ndiyo mchele unaotoa wali mtamu kuliko yote aliyoonja katika shindano hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags