Burna Boy aangukia kwenye uigizaji

Burna Boy aangukia kwenye uigizaji

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, Burna Boy ameripotiwa kuingia kwenye tasnia ya filamu kama mtayarishaji mkuu katika filamu iitwayo ‘3 Cold Dishes’.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo Burna atatayarisha filamu hiyo akishirikiana na kampuni ya filamu ya ‘Spaceship Films’, akiwa na meneja na mama yake mzazi Bose Ogulu.

Hii itakuwa filamu ya kwanza kwa Burna Boy baada ya kujitolea maisha yake kwenye muziki ambapo atashirikiana na baadhi ya mastaa wa filamu nchini humo akiwemo Asurf Oluseyi, mshindi wa Tuzo ya African Magic Viewer’s Choice (AMVCA) 2016, Wale Ojo, Osas Ighodaro, Femi Jacobs, pamoja na waigizaji wengine kutoka Ivory Coast na Senegal.

Burna Boy atakuwa ni mwanamuziki wa pili kuingia katika tasnia ya filamu kwa mwaka 2024 wa kwanza akiwa mwanadada Tiwa Savage na filamu yake iitwayo ‘Water and Garri’ ambayo ilianza kuoneshwa kwa mara ya kwanza Mei 10 kupitia Prime Video.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags